Uzamazao walitengeneza app hii kuwa ya bure. HUDUMA hii inatolewa bila gharama yoyote na imekusudiwa itumike kama ilivyo.
Ukurasa huu unatumika kuwahabarisha wageni kuhusu mwongozo wetu juu ya ukusanyaji, matumizi na utoaji habari Binafsi kama mtu yeyote akitaka kutumia huduma yetu.
Maneno yatumiwayo katika Mwongozo huu wa Siri Binafsi yana maana ile ile kama katika Masharti na Kanuni zetu, ambazo zinapatikana Uzamazao, isipokuwa kama yatafafanuliwa kivingine katika Mwongozo huu.
Ukusanywaji Habari Na Matumizi Yake
Ili kupata uzoefu bora wakati unapotumia Huduma yetu, tunaweza kukutaka utupe habari Fulani, ikiwa ni pamoja na za binafsi. Hii inaweza kuwa jina lako la kwanza na la pili, anwani yako ya barua pepe,namba yako ya simu, jina unalotumia kwenye mawasiliano ya kielektroniki, na hata mahali ulipo. Hiyo habari tutakayokuomba itahifadhiwa nasi na kutumiwa kama ilivyoelezwa katika ule mwongozo wetu wa Siri Binafsi.
App hii hutumia huduma za mtu/watu wa tatu zinazoweza kukusanya habari zilizotumiwa katika kukutambua.
Kiunganishi kwenda kwenye mwongozo wa Siri Binafsi wa huduma za mtu/watu wa tatu unaotumiwa na hii app.
Taarifa Kuhusu Matumizi Ya Data
Tunataka ujue kwamba kila unapotumia Huduma yetu, likitokea kosa katika app, tunakusanya data na habari (kupitia chombo cha huduma ya mtu/watu wa tatu) kwenye simu yako, kwa njia ya taarifa kuhusu matumizi ya data. Hizo taarifa zinaweza kuhusisha habari kama anwani ya Taratibu za intaneti za kifaa chako (“IP”), jina la chombo unachotumia, kizazi cha mfumo wa uendeshaji kifaa chako, mtiririko wa utendaji wa app wakati unapotumia Huduma yetu, muda na tarehe ya kutumika kwa huduma zetu, na takwimu zingine.
Cookies
“Cookies” ni faili zenye data kiasi kidogo ambazo kwa kawaida hutumiwa kama vitambulisho maalum, visivyokuwa wazi sana. Hutumwa kwenye mtambo wako wa kuchakata habari kutoka kwenye wavuti unazotembelea na huhifadhiwa kwenye eneo la kumbukumbu ndani ya kifaa chako.
Huduma yetu haitumii hizo “cookies” waziwazi. Lakini, app hii inaweza kutumia vidokezo vya mtu/watu wa tatu na maktaba zenye kutumia “cookies” ili kukusanya habari na kuboresha huduma zao. Una hiari ya kukubali au kuzikataa hizo “cookies” na fursa ya kujua ikiwa zinatumwa kwa kifaa chako. Ukiamua kuzikataa “cookies” zetu,unaweza kushindwa kutumia baadhi ya sehemu za hii Huduma.
Watoao Huduma
Sisi tunaweza kutumia makampuni mengine (mtu/watu wa tatu) na hata watoa huduma kwa sababu zifuatazo:
Tunataka kuwajulisha watumiaji wa hii Huduma kwamba hao makundi ya tatu wanaweza kupata habari zenu. Sababu ni ili waweze kufanya kazi walizopangiwa, kwa niaba yetu. Lakini, wanawajibika kuhifadhi na kutotoa habari hizo au kuzitumia kwa kusudi lingine lolote.
Usalama
Tunathamini Imani yako kwetu mpaka kutupa Habari zako Binafsi. Basi, tunajitahidi kutumia njia zote zinazokubalika kibiashara katika kulinda hizo habari. Lakini, kumbuka kwamba hakuna namna yoyote ya utumaji habari kwenye mtandao au uhifadhi wa kielektroniki ulio salama na wenye kuaminika asilimia mia moja. Hivyo hatuwezi kuhakikisha usalama kamili wa vitu hivyo.
Viunganishi Kwingine
Hii Huduma inaweza kuwa na viunganishi vya kukupeleka kwingine. Ukibonyeza kwenye kimojawapo, utapelekwa huko. Ona kwamba maeneo hayo ni nje ya huduma yetu, na hayaendeshwi nasi. Kwa hiyo, tunashauri upitie Miongozo yao kuhusu Maelezo ya Siri Binafsi. Sisi hatutawajibika kwa yaliyoko huko, miongozi yao, au utendaji wa huduma hizo ambazo si zetu.
Usalama Wa Watoto
Hizi huduma hazimhusu yeyote aliye chini ya umri wa miaka kumi na tatu (13). Hatukusanyi kwa kujua habari zozote binafsi kutoka kwa watoto walio chini ya miaka kumi na tatu (13). Tukija kugundua kwamba mtoto aliye chini ya miaka kumi na tatu (13) ametoa habari zake binafsi kwetu, mara moja tunazifuta kutoka mitamboni kwetu. Ikiwa wewe ni mzazi au ni mlezi, nawe unajua kwamba mtoto wako ametupa habari zake binafsi, tafadhali wasiliana nasi ili tuweze kuchukua hatua stahiki.
Mabadiliko Kwa Mwongozo Huu
Tunaweza kuufanyia marekebisho na maboresho Mwongozo huu mara kwa mara. Hivyo, unashauriwa kupitia ukurasa huu mara kwa mara ili kujionea mabadiliko yoyote. Tutakujulisha kuhusu mabadiliko yoyote kwa kuyaweka hayo mapya kwenye ukurasa huu.
Mwongozo Huu Umeanza Kutumika tarehe 1 mwezi wa Julai 2020.
Wasiliana Nasi
Ukiwa na maswali au mapendekezo yoyote kuhusu Mwongozo wetu wa Siri Binafsi, usisite kuwasiliana nasi kupitia anwani hii: ray.ruge@u zamazaol.com au abdulb@uzamazao.com
Ukurasa huu wa Mwongozo Binafsi ulitengenezwa kwenye tovuti hii:privacypolicytemplate.net